From Wikipedia, the free encyclopedia
Charles Martial Lavigerie (1825-1892) alikuwa askofu mkuu wa Algiers, Aljeria, na kardinali wa Kanisa Katoliki.
Ni maarufu hasa kwa kuanzisha mwaka 1868 shirika la Wamisionari wa Bibi Yetu wa Afrika (kifupi: Wamisionari wa Afrika, M. Afr.) linalojulikana kwa Kiingereza kama "White Fathers" (kwa Kifaransa "Pères Blancs"), kutokana na rangi ya kanzu yao.
Lengo lilikuwa hasa uinjilishaji wa bara la Afrika, na kweli wanashirika walijitosa kufanya kazi kubwa ambayo inaendelea hata leo, ambapo lina mapadri kama 1,500.
Kisheria ni shirika la maisha ya kitume. Wanashirika hawaweki nadhiri kama watawa, ila kiapo cha kufanya umisionari kwa Waafrika hadi kifo chao.
Kwa agizo la mwanzilishi wao wanatakiwa kuishi katika jumuia yenye wamisionari kutoka nchi mbalimbali na kutumia hata kati yao lugha ya wenyeji.
Barua yake ya mwaka 1886 kwa Papa Leo XIII inasema: "Wao wanataka utawala, utaalamu na uchumi. Sisi basi, tujitahidi kuleta Ukristo na uhuru wa kweli. Afrika iwe nchi ya Waafrika, nao Waafrika wasigeuzwe kuwa Wazungu weusi." [1].
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.