Channel O
From Wikipedia, the free encyclopedia
Channel O ni kituo cha muziki chenye makao yake Afrika Kusini ambayo ilianza kupeperusha vipindi kwa mara ya kwanza mapema katika miaka ya tisini. Wazo lake kuu ni muziki wa Kiafrika barani Afrika na ng'ambo. Katika miaka iliyopita, stesheni hii ya muziki imefanya majina ya watangazaji wake kujulikana sana kama vile Mimi, Nonhle, KB, Miss Candy.
Channel O inaweza kupatikana kupitia DSTV, hudumua ya Runinga ya kulipia kwa wakaazi takriban wote barani Afrika. Stesheni hii hupeperusha vipindi mbalimbali vya muziki kama vile Kwaito, Mbhaqanga , Injili (kutoka Afrika na ya Kimataifa), Hip hop, na mingine mingi. Huonyeshwa pia asubuhi katika Magicworld.
Pia huandaa mashindano ya kila mwaka ya Channel O Music Video Awards sherehe ambapo wasanii hutuzwa kwa mchango wao bora kwa muziki.