From Wikipedia, the free encyclopedia
Cecil John Rhodes (* 5 Julai 1853 Uingereza; † 26 Machi 1902 Afrika Kusini) alikuwa mfanyabiashara na mwanasiasa Mwingereza aliyetajirikia kutokana na malighafi za Afrika Kusini na kujenga himaya yake ya binafsi kati Afrika ya Kusini. Alianzisha koloni za Rhodesia ya Kaskazini na Rhodesia ya Kusini zilizokuwa baadaye Zambia na Zimbabwe.
Alikuwa kati ya wapangaji na watetezi wa ubeberu wa Uingereza katika karne ya 19. Aliamini ya kuwa Waingereza ni mbari wa juu duniani.
Alizaliwa Bishop's Stortford (Uingereza) akiwa mtoto wa mchungaji wa kanisa. 1870 wazazi walimtuma kijana kwenda Afrika Kusini kwa shabaha ya kuboresha afya yake akiwa na matatizo kutokana na hali ya hewa Uingereza. Baada ya kufika alijishughulisha na biashara ya migodi ya almasi ya Kimberley (Afrika Kusini) akatajirika haraka. Akarudi Uingereza akasoma kwenye chuo kikuu cha Oxford lakini alipaswa kurudi Afrika kwa sababu ya afya. Akajiunga na siasa akawa mbunge wa koloni ya rasi tangu 1881.
1880 alianzisha kampuni yake ya binafsi ya De Beers iliyopata baadaye nafasi ya kwanza katika biashara ya almasi duniani.
Athira yake ya kisiasa ikapanuka 1885 akashawishi serikali ya London kuvamia eneo la Bechuanaland (Botswana) na kuifanya nchi lindwa chini ya Uingereza.
1885 alifaulu kupata kibali cha serikali ya Uingereza kuanzisha koloni ya binafsi kaskazini ya Afrika kusini. Akaunda Kampuni ya Kiingereza ya Afrika Kusini (British South Africa Company) na kuvamia maeneo ya Zambia na Zimbabwe ya leo. Ardhi iliyotwaliwa iliuzwa kwa walowezi na koloni za kampuni ziliitwa Rhodesia ya Kaskazini na Rhodesia ya Kusini. Zilikaa chini ya kampuni ya Rhodes hadi 1923 zikachukuliwa baadaye na serikali ya Uingereza.
1890 Rhodes akawa waziri mkuu wa koloni ya Rasi. Kama kiongozi wa serikali alitaka kumeza jamhuri ya makaburu ya Transvaal na akajaribu kumpindua raisi Ohm Krueger 1895. Shambulio ya Jameson Raid ilishindikana na Rhodes alipaswa kujiuzulu katika serikali.
Akaendelea kukaza ukoloni wake huko Rhodesia hadi kifo chake mwaka 1902.
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.