Byzacena
From Wikipedia, the free encyclopedia
Byzacena (au Byzacium; kwa Kigiriki: Βυζάκιον bizakion) [1] lilikuwa jimbo la Kiroma kwenye karne za mwisho wa Dola la Roma katika Afrika Kaskazini. Kwa asili lilikuwa sehemu ya Afrika ya Kiroma iliyogawiwa na Kaizari Diokletian mnamo mwaka 293; Byzacea ililingana takriban na Tunisia ya kusini mashariki ya leo.
Makao makuu ya jimbo jilo jipya yalipelekwa kwenye mji wa Hadrumetum (Sousse ya leo). Katika kipindi hicho, jimbo la Kanisa la Byzacena lilikuwa katika nafasi ya tatu kwa umuhimu katika Afrika baada ya Patriarki wa Aleksandria (Misri) na askofu mkuu wa Karthago.