Buruji za falaki
From Wikipedia, the free encyclopedia
Buruji za falaki (pia: alama za nyota; kwa Kiingereza: zodiac constellations) ni jina la makundinyota yanayoonekana kwenye ekliptiki zaani njia ya Jua angani (ing. ecliptic) na kuunda Zodiaki.
![Thumb image](http://upload.wikimedia.org/wikipedia/commons/thumb/a/a1/Book_of_the_Fixed_Stars_Auv0280_Sagittarius.jpg/640px-Book_of_the_Fixed_Stars_Auv0280_Sagittarius.jpg)
Katika maarifa ya unajimu (au: falaki, tofauti na fani ya sayansi inayoitwa astronomia) Waswahili wa kale, pamoja na tamaduni nyingi za zamani, waliamini ya kwamba nyota hizi zina tabia fulani na kuwa na athari juu ya maisha ya binadamu wanaozaliwa chini ya nyota fulani.
Hali halisi Jua linapita katika maeneo ya makundinyota 13 lakini tangu zamani za Babeli idadi ilifupishwa kuwa 12 kwa kusudi la kulingana na kalenda ya miezi 12. Kwa kufikia idadi hii kundinyota la Hawaa (Ophiuchus) liliondolewa katika idadi ya Zodiaki.