Boga
From Wikipedia, the free encyclopedia
Maboga au malenge ni matunda ya mboga (pia mlenge) yenye umbo la kibuyu katika familia Cucurbitaceae. Matunda haya hutoka kwenye spishi mbalimbali katika jenasi Coccinia, Cucurbita na Momordica. Maboga huwa na rangi ya manjano, ya machungwa au ya majani na huwa na mikunjo kuanzia kwenye shina juu mpaka chini. Maboga yana kombe / ganda nene huku mbegu na nyama ya tunda ikiwa ndani.