Bartolomeo Kijana
Mtakatifu wa Kiitalia / From Wikipedia, the free encyclopedia
Bartolomeo Kijana (Rossano Calabro, mkoa wa Calabria, Italia, 981 – Grottaferrata, karibu na Roma, 1055) alikuwa abati wa monasteri ya Ukristo wa Mashariki aliyoianzisha pamoja na mwalimu wake, Nilo wa Rossano[1].
Kati ya maandishi yake, muhimu zaidi ni kitabu cha maisha ya mwalimu wake huyo.
Tangu kale anaheshimiwa na Kanisa Katoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu.
Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 11 Novemba[2].