![cover image](https://wikiwandv2-19431.kxcdn.com/_next/image?url=https://upload.wikimedia.org/wikipedia/commons/thumb/0/01/East_China_Sea_Map.jpg/640px-East_China_Sea_Map.jpg&w=640&q=50)
Bahari ya Mashariki ya China
From Wikipedia, the free encyclopedia
Bahari ya Mashariki ya China (ing. East China Sea) ni bahari ya pembeni iliyopo kando ya mashariki mwa nchi ya China, pamoja na Bahari ya Njano na Bahari ya Kusini ya China.[1] [2]
![Thumb image](http://upload.wikimedia.org/wikipedia/commons/thumb/0/01/East_China_Sea_Map.jpg/320px-East_China_Sea_Map.jpg)
Bahari hiyo ni sehemu ya Bahari Pasifiki na ina eneo la kilomita za mraba zipatazo 1,249,000. Nchini China, bahari hii inaitwa Bahari ya Mashariki.
Nchini Korea Kusini, bahari hii kuna kipindi huitwa Bahari ya Kusini, lakini hii mara nyingi hutumiwa kutajia eneo la karibu na pwani ya kusini mwa nchi ya Korea Kusini.