Areopago
From Wikipedia, the free encyclopedia
From Wikipedia, the free encyclopedia
Areopago(kutoka Kigiriki Ἄρειος Πάγος) ni mwamba uliotokeza juu ya Akropoli ya Athens, mji mkuu wa Ugiriki.
Ilitumika kama mahakama[1] na kama mahali pa midahalo ya kifalsafa.
Kwa sababu hiyo Mtume Paulo alipotaka kuhubiri Ukristo alialikwa kwenye Areopago. Hotuba hiyo maarufu inapatikana katika Mdo 17.
"Areopago mamboleo" inamaanisha mitandao na vyombo vya habari ambavyo ni uwanja mpya wa kuwasiliana na kueneza mawazo kati ya watu wa nyakati hizi.