Antili za Kiholanzi
From Wikipedia, the free encyclopedia
Antili za Kiholanzi ni visiwa kadhaa katika Bahari ya Karibi kati ya Puerto Rico na pwani ya Venezuela (Amerika Kusini) vinavyohesabiwa kati ya visiwa vya Antili Ndogo.
Ukweli wa haraka
| |||||
Kaulimbiu ya taifa: Libertate unanimus (Kilatini: "Umoja kwa uhuru") | |||||
Wimbo wa taifa: Our islands in the sea | |||||
Mji mkuu | Willemstad (Curacao) 12°7′ N 68°56′ W | ||||
Mji mkubwa nchini | Willemstad (Curacao) | ||||
Lugha rasmi | Kiholanzi | ||||
Serikali | Beatrix wa Uholanzi Frits Goedgedrag Emily de Jongh-Elhage | ||||
Ufalme wa kikatiba |
|||||
Eneo - Jumla - Maji (%) |
960 km² (ya 184) | ||||
Idadi ya watu - Julai 2005 kadirio - Msongamano wa watu |
183,000 (ya 185) 229/km² (ya 51) | ||||
Fedha | Gulden ya Antili za Kiholanzi (ANG ) | ||||
Saa za eneo - Kiangazi (DST) |
(UTC-4) (UTC) | ||||
Intaneti TLD | .an | ||||
Kodi ya simu | +599
- |
Funga
Visiwa vitano hukaliwa na watu, kuna vingi vingine vidogo. Vyote vilikuwa makoloni ya Uholanzi ila sasa vimekuwa sehemu za Ufalme wa Nchi za Chini katika hali mbalimbali za kisheria.
Visiwa hivyo kijiografia wanagawanyika kati ya:
- Visiwa vya Windward ("penye upepo") viko karibu na Puerto Rico
- Saba
- Sint Eustatius, kwa lugha ya wenyeji: Statia
- Sint Maarten (kusini tu mwa kisiwa; kaskazini ni eneo la Ufaransa chini ya mkoa wa Guadeloupe)