Anthropolojia ya Kimarekani
From Wikipedia, the free encyclopedia
Anthropolojia ya Kimarekani ni aina ya anthropolojia inayozingatia hasa wazo la utamaduni ambao ulifafanuliwa kama uwezo wa kiubia wa binadamu wa kuainisha na kusimbika tajiriba zao kiishara na kuwasilisha kiishara tajiriba zilizosimbikwa kijamii.
Anthropolojia ya Kimarekani imepangiliwa katika mawanda manne. Kila mojawapo huchangia sana utafiti wa utamaduni. Mawanda yenyewe ni: anthropolojia ya kibiolojia, isimu, anthropolojia ya kiutamaduni, na akiolojia. Utafiti katika mawanda hayo umewaathiri kwa kiwango fulani wanaathropolojia wanaofanya kazi katika nchi nyingine.