mwanasiasa kutoka nchini tanzania From Wikipedia, the free encyclopedia
Anna Kajumulo Tibaijuka (alizaliwa 12 Oktoba, 1950) ni mtaalamu wa Uchumi wa kilimo, pia mwanasiasa wa Tanzania katika CCM na alikuwa Mbunge wa jimbo la Muleba Kusini tangu mwaka 2010 hadi 2020.
Profesa Anna Tibaijuka Mbunge | |
Muda wa Utawala 28 Novemba 2010 – 23 Disemba 2014 | |
Rais | Jakaya Kikwete |
---|---|
mtangulizi | John Zefania Chiligati |
Mkurugenzi Mtendaji wa UN–HABITAT | |
Muda wa Utawala Machi 2006 – 2010 | |
aliyemfuata | Joan Clos i Matheu |
Mbunge kwa Muleba Kusini | |
Muda wa Utawala Novemba 2010 – November 2020 | |
mtangulizi | Wilson Masilingi |
aliyemfuata | Oscar Ishengoma Kikoyo |
Majority | Unopposed |
tarehe ya kuzaliwa | 12 Oktoba 1950 Kagabiro, Muleba, Tanganyika |
utaifa | Mtanzania |
chama | CCM |
watoto | 4 |
mhitimu wa | Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo Chuo Kikuu cha Sayansi ya Kilimo, Uppsala, Uswidi |
Awards | Gothenburg Award |
tovuti | annatibaijuka.org |
Aliwahi kuwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi. [1]
Alizaliwa Kagabiro karibu na Muleba, Tanzania katika familia ya wakulima wadogo.
Miaka 1958-1961 alisoma shule ya msingi Kaigara akaendelea kwenye shule ya kati ya Wasichana ya Kashozi – Kamukukubwa halafu shule ya sekondari ya wasichana Rugambwa, Bukoba, 1966 – 1969. Kutoka hapo alipokewa Form V ya Marian Girls, Morogoro.
Baada ya huduma kwenye Jeshi la Kujenga Taifa akajiunga na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Kitivo cha Kilimo, Morogoro 1972 - 1975 hadi digrii ya kwanza. Akaajiriwa kama Mhadhiri Mzaidizi kwenye Idara ya Uchumi. Mwaka huohuo akafunga ndoa na Wilson Kamuhabwa Tibaijuka, aliyekuwa kwa wakati huo afisa katika ubalozi wa Tanzania nchini Uswidi.[2] Alizaa naye watoto wanne, Muganyizi (1976), Kemilembe (1979), Kagemulo (1986) na Kankiza (1991). Wakati wa kukaa Uswidi alisoma hadi digrii ya pili kwenye Chuo Kikuu cha Kilimo, Uppsala.
Mwaka 1979 familia ilirudi Tanzania na Anna Tibaijuka alianza kufundisha kwenye Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Kitengo cha Utafiti wa Uchumi. 1981 alifadhiliwa kurudi Uswidi na kufuata kozi ya PhD aliyomaliza 1983. Akarudi Dar es Salaam akafundisha tena uchumi.
Mwaka 1998 aliteuliwa kujiunga na ofisi kuu ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Biashara na Maendeleo (UNCTAD) mjini Geneva alikoongoza idara ya nchi maskini. Baada ya miaka miwili huko Geneva aliombwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Kofi Annan kuongoza Kituo cha Makazi Duniani (UN-Habitat Centre). Alifanya mabadiliko na matengenezo katika kazi ya kituo hii hadi Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa uliamua kupandisha hadhi ya kituo kuwa "United Nations Human Settlements Programme" (UN-HABITAT) yenye makao makuu huko Nairobi. Tibaijuka alichaguliwa kuwa mkurugenzi mtendaji wa kitengo hiki kipya mwaka 2002 akapewa cheo cha Katibu Mkuu Msaidizi na hapo alikuwa mwanamke Mwafrika wa kwanza aliyefika ngazi hii katika historia ya UM hadi leo (2017).
Mwaka 2010 alirudi Tanzania baada ya kumaliza kipindi chake cha pili cha kuongoza UN-HABITAT. Alishiriki katika uchaguzi mkuu akachaguliwa mbunge wa Muleba Kusini kwa niaba ya CCM.
Baada ya uchaguzi aliingia katika serikali ya Mizengo Pinda akiwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi. Mwezi wa Desemba 2014 rais Jakaya Kikwete alimwachisha Tibaijuka kutoka wizara yake kwa sababu aliwahi kupokea pesa kutoka James Rugemalira wa VIP Engineering and Marketing (VIPEM) aliyehusika katika kashfa ya rushwa ya Tegeta escrow. [3]. Alikosolewa kwa kupokea milioni 1 ya USD kwenye akaunti yake ya binafsi.
Tibaijuka alijaribu kujitetea kuwa pesa ilikuwa msaada kwa ajili ya taasisi ya Joha Trust inayogharimia shule ya wasichana ya Barbro Johansson na ya kwamba pesa ilipitia tu katika akaunti yake ya binafsi.[4]
Mwaka 2015 alipendelewa tema kugombea ubunge wa Muleba Kusini kwa kura ya maoni ya asilimia 63% za wana CCM wa jimbo[5][6]. Akashinda uchaguzi akarudi bunge la Tanzania.[7]
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.