mwanasiasa Mjerumani From Wikipedia, the free encyclopedia
Aminata Touré (amezaliwa 15 Novemba 1992) ni mwanasiasa Mjerumani wa chama cha Alliance '90/The Greens. Alichaguliwa tarehe 29 Juni 2017 kuwa mbunge wa kijimbo wa Schleswig-Holstein. Alikuwa kijana wa miaka 25 wakati wa uchaguzi alihudumu kama makamu wa spika wa bunge hadi 2022. [1] [2] [3] Mwaka 2022 aliteuliwa kuwa waziri wa Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto wa Jimbo la Schleswig-Holstein.
Aminata Touré | |
Touré in 2018 | |
Member of the Bunge la Schleswig-Holstein | |
Aliingia ofisini 29 June 2017 | |
Vice-President of the Bunge la Schleswig-Holstein | |
Muda wa Utawala 28 August 2019 – 07 June 2022 | |
tarehe ya kuzaliwa | 15 Novemba 1992 Neumünster, Ujerumani |
---|---|
utaifa | Ujerumani |
chama | Chama cha Kijani cha Ujerumani |
mhitimu wa | Chuo Kikuu cha Kiel |
tovuti | aminata-toure.de |
Wazazi wa Touré walikimbilia Ujerumani kufuatia mapinduzi ya kijeshi nchini Mali ya 1991 . [4] [5] Alizaliwa 1992 huko Neumünster, Ujerumani. Mwaka 2011 alihitimu mitihani ya Abitur (Form VI ya Ujerumani) akaendelea kusoma Elimu ya Siasa na Kifaransa katika Chuo Kikuu cha Kiel hadi kupata Awali mwaka wa 2016. [6] Wakati wa masomo yake alisoma mwaka mmoja kwenye Chuo Kikuu cha Complutense cha Madrid. Kuanzia 2014 hadi 2017, alifanya kazi kama msaidizi katika ofisi ya mbunge Luise Amtsberg .
Mnamo 2012, Touré alijiunga na Vijana wa Chama cha Kijani akachaguliwa kama mwenyekiti a umoja huo mjini Kiel.
Mnamo 2016, aliingia katika kamati ya kijimbo cha chama na mwaka 2017 alichaguliwa kama mbunge wa bunge la kijimbo.
Mwaka 2019 alichaguliwa kuwa makamu wa spika wa bunge hilo.[7] Alikuwa Mjerumani Mwafrika wa kwanza na pia kijana wa kwanza kushika nafasi ya aina hii katika mabunge yote ya Ujerumani.[8]
Mwaka 2022 alirudishwa kwenye bunge la jimbo akateuliwa kuwa waziri katika serikali ya ushirikiano na chama cha CDU.
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.