![cover image](https://wikiwandv2-19431.kxcdn.com/_next/image?url=https://upload.wikimedia.org/wikipedia/commons/thumb/e/e8/Ethanol-structure.svg/langsw-640px-Ethanol-structure.svg.png&w=640&q=50)
Ethanoli
From Wikipedia, the free encyclopedia
Ethanoli (pia: alkoholi ethili) ni dawa lililopo ndani ya aina zote za vinywaji vya pombe.
![Thumb image](http://upload.wikimedia.org/wikipedia/commons/thumb/e/e8/Ethanol-structure.svg/320px-Ethanol-structure.svg.png)
![Thumb image](http://upload.wikimedia.org/wikipedia/commons/thumb/2/26/Ethanol_-_Space_filling_model.png/640px-Ethanol_-_Space_filling_model.png)
![Thumb image](http://upload.wikimedia.org/wikipedia/commons/thumb/0/0f/Ethanol_Flasche.jpg/320px-Ethanol_Flasche.jpg)
Kikemia ni kampaundi ogania inayopatikana kama kiowevu kisicho na rangi. Ikiwa ni dawa safi inawaka haraka lakini mara nyingi hupatikana kama mchanganyiko pamoja na maji katika aina za pombe; hapa inawaka tu kama asilimia yake inapita kiwago cha 60%.
Fomula yake ni C2H5OH inayoandikwa pia C2H6O. Ni dawa lenye tabia ya sumu kiasi kwa mwili wa kibinadamu pia ina tabia ya kuyeyusha.