Alfa na Omega
From Wikipedia, the free encyclopedia
Alfa (Α au α) na omega (Ω or ω) ndizo herufi ya kwanza na ya mwisho ya alfabeti ya Kigiriki.
Kwa sababu hiyo zimechukuliwa kama ishara ya mwanzo na mwisho.
Kitabu cha Ufunuo (1:8, 21:6 na 22:13)[1] kinazitumia pamoja kama jina la Yesu Kristo na la Mungu[2][3], kwa kuwa ndio asili na kikomo cha viumbe vyote.