Alazeya
From Wikipedia, the free encyclopedia
Alazeya (kwa Kirusi: Алазея) ni mto ulioko Urusi; una urefu wa kilometa 1,590 na kupita katika tundra.
Beseni la Alazeya ni la km² 64,700 liko katika Yakutia, eneo kubwa la Siberia kwenye mashariki ya Urusi upande wa Asia.
Alazeya inaanza pale ambako mito ya Nelkan na Kadylchan inaungana ikiishia kwenye Bahari ya Mashariki ya Siberia.
Kuanzia Oktoba hadi Mei au Juni maji yake huganda kuwa barafu.