Ajira kwa watoto
unyonyaji wa watoto kupitia aina yoyote ya kazi / From Wikipedia, the free encyclopedia
Ajira kwa watoto inarejelea unyonyaji wa watoto kupitia aina yoyote ya kazi ambayo inawanyima utoto wao, inaingilia uwezo wao wa kuhudhuria shule ya kawaida, na inawadhuru kiakili, kimwili, kijamii na kimaadili.[3] Unyonyaji kama huo umepigwa marufuku na sheria duniani kote, [4] ingawa sheria hizo hazihesabu kazi zote za watoto kama ajira yao; kwa mfano kazi za usanii, majukumu ya familia, mafunzo yanayosimamiwa, na baadhi ya aina za kazi za watoto zinazofanywa kimalezi.[5] [6] Umaskini na ukosefu wa shule vinachukuliwa kuwa sababu kuu ya ajira kwa watoto. [7]