From Wikipedia, the free encyclopedia
Adıyaman (kwa Kizazaki: Semsur) (Perre ya kale au Pordonnium) ni mji uliopo kusini-mashariki mwa nchi ya Uturuki, na pia ni mji mkuu wa Mkoa wa Adıyaman.
Ni mmoja kati ya miji inayokua haraka zaidi katika nchi ya Uturuki. Idadi ya wakazi wa huko inaanzia 100,045 (1990) hadi 178,538 (2000) (kwa mujibu wa sensa zao).
Mwanzoni mji ulikuwa na jina la Kiarabu 'Hisnimansur' likiwa kama jina rasmi la mji hadi kufikia mwaka 1926, lakini jina hilo likawa gumu kwa watu wa Uturuki kulitamka, na badala yake wakawa wanalifupisha na kuliita 'adi yaman' likiwa na maana ya 'jina gumu' au '(eneo) la jina gumu katika Uturuki. Mnamo 1926, jina hilo likawa ndilo jina kamili la mji huu.
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.