Zoilo wa Cordoba
From Wikipedia, the free encyclopedia
Zoilo wa Cordoba (alifariki Cordoba, 304) alikuwa Mkristo wa Hispania, aliyeuawa pamoja na wenzake 19[1] mwanzoni mwa dhuluma ya kaisari Diokletian [2].
Tangu kale anaheshimiwa na Kanisa Katoliki na Kanisa la Kiorthodoksi kama mtakatifu mfiadini.
Sikukuu yake inaadhimishwa kila tarehe 27 Juni[3] au 22 Desemba[4].