Papa Leo III
From Wikipedia, the free encyclopedia
Papa Leo III (takriban 750 – 12 Juni 816) alikuwa Papa kuanzia tarehe 26/27 Desemba 795 hadi kifo chake[1]. Alitokea Roma, Lazio, Italia[2].

Alimfuata Papa Adriano I akafuatwa na Papa Stefano IV.
Alitetea kwa kila njia imani sahihi na hasa umungu wa Yesu Kristo.
Leo III amejulikana hasa kwa tendo lake la kumtia Karolo Mkuu taji la Kaisari wa Roma tarehe 25 Desemba mwaka 800.
Leo III alitangazwa na Papa Klementi X kuwa mtakatifu mwaka 1673.
Maisha
Mwenyewe alizaliwa katika familia ya kawaida, akaona upinzani mkali baada ya uchaguzi wake kutoka familia za makabaila wa mji wa Roma waliojaribu kumwua kwa sababu walizoea kuwa na athira juu ya uchaguzi wa Papa wakati ule.
Hivyo Leo alikimbia hadi Ujerumani akitafuta msaada wa Karolo Mkuu mfalme wa Wafaranki. Karolo alimrudisha Roma na walinzi, akafika mwenyewe kuchungulia mashtaka dhidi ya Leo III akaona yalikuwa ya uongo.
Leo III kwa upande wake alijaribu kuimarisha uhusiano wake na Karolo kwa kumvika taji la Kaisari. Hivyo Karolo alikuwa mtu wa kwanza wa kutumia cheo hicho katika mji wa Roma tangu 476, mwaka Kaisari wa mwisho Romulus Augustus alipofukuzwa, na cheo cha Kaisari wa Roma kilipatikana huko Konstantinopoli tu kwa mtawala wa Bizanti.
Tendo la kumwekea Karolo taji hilo lilimkasirisha kiongozi wa Konstantinopoli lakini alikosa nguvu ya kuadhibu Papa au Karolo.
Hivyo Leo III alianzisha ufuatano wa makaisari wa "Dola Takatifu la Kiroma" ulioendelea hadi mwaka 1804.
Tazama pia
Maandishi yake
- Opera Omnia katika Patrologia Latina ya Migne pamoja na faharasa
Tanbihi
Viungo vya nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.