Nyama choma
From Wikipedia, the free encyclopedia
Nyama choma ni nyama iliyopikwa kwa kuchomwa kwa moto, makaa au jiko la umeme. Pia nyama inaweza kuchomwa na majiko maalum ya kisasa ya gesi ya kuchomea nyama.
Nyama inaweza ama kuchomwa moja kwa moja, ama kwanza kuchemshwa au kupikwa na moshi, mtindo maarufu hasa Marekani, kabla ya kuchomwa.
Harufu yake inavutia watu wengi kuipenda katika nchi na tamaduni mbalimbali duniani. Hivyo imekuwa biashara hasa katika barabara za mijini.
Nyama hii hupendwa pia wakati wa sherehe, matukio muhimu ya kifamilia na marafiki au mwisho wa wiki kwa wale wanaokunywa pombe. Pamoja na kuliwa na vyakula vingine, mara nyingi huandaliwa na kachumbari.