Lazaro wa Bethania
From Wikipedia, the free encyclopedia
Lazaro (kwa Kiebrania אלעזר, Eleazar au Eliezer) ni mtu anayetajwa katika Injili ya Yohane: aliishi katika karne ya 1 huko Bethania, kijiji karibu na Yerusalemu, pamoja na dada zake Martha na Maria.
Maelezo zaidi Mfululizo wa kurasa juu ya Yesu, Mazingira ya Yesu ...
Funga
Yesu Kristo alifurahia urafiki wao wote, hasa alipokuwa akihiji kwenda Yerusalemu.
Katika nafasi ya mwisho ya kufanya hivyo, alimfufua siku ya nne baada ya kifo chake, jambo lililofanya wengi wamuamini kuwa ndiye Kristo, lakini pia wapinzani wake waharakishe kifo chake mwenyewe[1].
Lazaro anaheshimiwa na Kanisa Katoliki, na Waorthodoksi na wengineo kama mtakatifu.
Sikukuu yake huadhimishwa pamoja na ya dada zake[2] tarehe 29 Julai[3].