Gall Mtakatifu
From Wikipedia, the free encyclopedia
Gall, Gallech, Gallen au Gallus (550 hivi - 646 hivi) alikuwa padri mmonaki, mwanafunzi wa Kolumbani akamfuata kutoka Ireland kwenda kuinjilisha sehemu mbalimbali za Ulaya Bara akaishia katika Uswisi wa leo[1][2][3][4].
Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu.