Adelino wa Celles
From Wikipedia, the free encyclopedia
Adelino wa Celles (pia: Hadelinus; alifariki 690 hivi[1]) kwanza alifanya kazi ikulu[2] , halafu akawa mmonaki, padri, mmisionari, mwanzilishi wa monasteri na hatimaye mkaapweke[3].
Alifanya kazi ya kueneza Injili hasa Ubelgiji, akishirikiana na mwalimu wake, askofu Remakli[4] .
Tangu kale ameheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu[5].
Sikukuu yake ni tarehe 3 Februari[6].