Welisi

nchi ya visiwa katika Ulaya Kaskazini-Magharibi, sehemu ya Ufalme wa Muungano From Wikipedia, the free encyclopedia

Welisi

Welisi ni nchi katika Ufalme wa Muungano, iliyoko kwenye kisiwa cha Britania Kuu. Inapakana na Uingereza upande wa mashariki, huku Bahari ya Eire ikiwa kaskazini na magharibi, na Mfereji wa Bristol upande wa kusini. Nchi hii ina eneo la takriban 20,779 km² (8,023 sq mi) na ina idadi ya watu milioni 3.2. Cardiff ni mji mkuu na jiji lake kubwa zaidi, likihudumu kama kituo cha utawala na uchumi. Kiingereza na Kiwelisi ndizo lugha rasmi, na urithi wake wa kiutamaduni una mizizi katika asili yake ya Kikelti. Nchi hii ina serikali yenye mamlaka ya ndani, ikiwa na mamlaka ya kutunga sheria kupitia Senedd (Bunge la Welisi) katika nyanja kama afya, elimu, na usafiri, huku ikiendelea kuwa sehemu ya Ufalme wa Muungano.

Ukweli wa haraka
'Cymru
Welisi (Wales)
Thumb Thumb
Bendera Nembo
Kaulimbiu ya taifa: Cymru am byth (Kiwelisi)
"Welisi milele"
Wimbo wa taifa: Hen Wlad Fy Nhadau (Kiwelisi)
Nchi ya mababu yangu
Thumb
Mji mkuu Cardiff
51°29 N 3°11 W
Mji mkubwa nchini Mji mkuu
Lugha rasmi Kiwelisi, Kiingereza
Serikali
Mfalme
Waziri Mkuu wa Ufalme
Waziri kiongozi wa Wales
Ufalme wa Kikatiba
Charles III wa Uingereza
Rishi Sunak
Mark Drakeford
Muungano wa Welisi
Mfalme Gruffudd ap Llywelyn
1056
Eneo
 - Jumla
 - Maji (%)
 
20,779 km² ()
Idadi ya watu
 - 2017 kadirio
 - 2011 sensa
 - Msongamano wa watu
 
3,124,0001 ()
3,063,456
140/km² ()
Fedha Pound sterling (GBP)
Saa za eneo
 - Kiangazi (DST)
GMT (UTC0)
BST (UTC+1)
Intaneti TLD .uk2
Kodi ya simu +44

-

Funga


Thumb
Ramani ya Welisi

Welisi ina historia tajiri, ikiwa na wakazi wa kwanza wa Britoni wa Kikelti kabla ya kuingizwa katika Ufalme wa Uingereza kupitia Sheria za Welisi (1535–1542). Licha ya muungano huo, Welisi imehifadhi utambulisho wake wa kitaifa, huku juhudi za kuhifadhi na kukuza lugha ya Kiwelisi na tamaduni zake zikiendelea.

Historia

Welisi ilikaliwa na makabila mbalimbali ya Kikelti wakati kisiwa cha Britania kilivamiwa na Dola la Roma katika karne ya 1 BK. Waroma walitawala hadi mnamo mwaka 400 BK.

Tangu kuingia kwa Waanglia-Saksoni kisiwani na uenezi wao katika karne ya 5 milima ya Welisi ilibaki eneo ambako utamaduni wa Wakelti uliendelea kustawi.

Kuanzia mwaka wa 1284 Welisi ilivamiwa na Uingereza na kuunganishwa kama sehemu kamili ya Ufalme wa Uingereza mwaka 1536.

Baada ya Ufalme wa Uingereza kuungana na Uskoti na Eire Welisi ilitambuliwa kama sehemu asilia ya Ufalme wa Muungano.

Katika karne ya 18 na 19 Welisi iliona kuongezeka kwa viwanda; makaa mawe na migodi ya shaba na chuma viliweka msingi wa tasnifu ya viwanda. Viwanda vya Welisi vilizalisha karibu nusu ya chuma chote cha Uingereza. Wakazi waliongezeka hasa kusini kwa sababu wafanyakazi Waingereza walihamia Welisi.

Katika karne ya 20 akiba za malighafi zilikwisha na viwanda vingi vilifungwa.

Mwaka wa 1998 Welisi ilipewa bunge lake la pekee linalosimamia matumizi ya makisio yake na kuchagua serikali ya eneo.

Watu

Idadi ya wakazi ni zaidi ya milioni tatu.

Lugha asilia ni Kiwelisi ambacho ni kimoja kati ya lugha za Kikelti. Leo hii kuna bado asilimia 19 za wakazi wanaotumia Kiwelisi lakini wengine wamezoea zaidi Kiingereza. Wasemaji wa Kiwelisi wako hasa kaskazini na kwenye sehemu ya milima ambako kuna maeneo ambako idadi kubwa ya watu huongea lugha hii wakijua Kiingereza kama lugha ya pili.

Upande wa dini, 57.6% ni Wakristo, hasa Waanglikana. 0.8% ni Waislamu. 32.1% hawana dini yoyote.

Makala hii kuhusu maeneo ya Ulaya bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Welisi kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.