Wakati huo waligawanyika kati ya Wathervingi na Wagreuthungi. Miaka ya 300, Ermanariki, mfalme wa Wagreuthungi, alitawala kutoka Bahari ya Baltiki hadi Bahari Nyeusi, na Milima ya Urali. Wakati huo wengi wao waliingia Ukristo wa madhehebu ya Uario kwa umisionari wa Ulfilas, aliyebuni alfabeti ya Kigoti kuandika Biblia ya Kigoti.
Miaka ya 370 maeneo ya Wagoti yalivamiwa na Wahunni. Wagreuthungi wakakaa chini yao wakaja kuitwa Waostrogoti, kumbe Wathervingi, waliojulikana baadaye kama Wavisigoti, walivuka mtoDanube na kuvamia Dola la Roma. Baada ya kunyanyaswa sana, waliasi na kushinda Warumi katika Mapigano ya Adrianopolimwaka378. Chini ya Alariki I, waliteka Roma yenyewe mwaka 410, na hatimaye wakalowea Galia na Hispania, walipounda Ufalme wa Wavisigoti.
Wakiungana na Dola la Roma Magharibi dhidi ya Wahunni wa Attila na Waostrogoti walipata ushindi kwenye Mapigano ya Uwanja wa Katalauni mwaka 451. Hapo Waostrogoti walijinasua katika utawala wa Wahunni wakavamia Italia mwishoni mwa karne ya 5 chini ya mfalme Theodoriki Mkuu, wakaanzisha Ufalme wa Waostrogoti.
Amory, Patrick. People and Identity in Ostrogothic Italy, 489–554. Cambridge: Cambridge University Press, 2003. ISBN 0-521-52635-3.
Backman, Clifford R (2008). The Worlds of Medieval Europe. Oxford and New York: Oxford University Press. ISBN978-0-19-533527-9. {{cite book}}: Invalid |ref=harv (help)
Frassetto, Michael (2003). Encyclopedia of Barbarian Europe: Society in Transformation. Santa Barbara, CA: ABC-CLIO. ISBN978-1-57607-263-9. {{cite book}}: Invalid |ref=harv (help)
Larned, J. N., ed. (1895). History for Ready Reference. Cambridge, MA: C.A. Nichols. {{cite book}}: |first= has generic name (help); Invalid |ref=harv (help)CS1 maint: multiple names: authors list (link)
Makala hii kuhusu mambo ya kihistoria bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Waostrogoti kama enzi zake au matokeo yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Wikiwand in your browser!
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.