Remove ads
From Wikipedia, the free encyclopedia
Vyakula vya Ethiopia kwa kawaida vina milo ya mboga ambayo ina manukato na nyama, na kwa kawaida huwa katika fomu ya wat (au wot ), kitoweo ambacho ni nzito , kinachopakuliwa juu ya Injera, mkate mkubwa wa kinyunga, ambao wapata sentimita 50 (inchi 20) katika kipenyo na umetengenezwa kutoka unga wa teff uliowachwa kukaa kwa muda mrefu (ferment). Waethiopia hula kwa mikono yao ya kulia, na hutumia vipande vya Injera kuchukua vipande vya entrées na milo ya kando Hakuna vyombo vinavyotumika.
Vyakula vya kitamaduni vya Ethiopia havihusishi nyama ya aina yoyote ya nguruwe, kwani Waethiopia wengi ni Wakristo wa kanisa ya Orthodox, Waislamu au Wayahudi, na hivyo basi wamepigwa marufuku kula nyama ya nguruwe Aidha, Kanisa ya Orthodox ya Ethiopia hupeana idadi ya vipindi vya kufunga (tsom Ge'ez: ጾም tṣōm ), vinavyojumuisha siku za Jumatano, Ijumaa, na msimu nzima wa Kwaresima, kwa hivyo vyakula vya Ethiopia vina mboga nyingi (Kiamhariki: ye-tsom የጾም ye-Som , Kitigrinya: Bali-tsom ናይጾም Bali-Som). Hii imepelekea wapishi wa Ethiopia kutengeneza vyanzo vingi vya mafuta ya kupikia: pamoja na sesame na safflower, vyakula vya Ethiopia pia hutumia nug (pia yatamkwa noog , pia inajulikana kama mbegu ya niger ). Mikahawa ya Ethiopia ni chaguo maarufu kwa walaji mboga wanaoishi katika nchi za Magharibi.
Berbere , ambayo ni mchanganyiko wa pilipili ya poda ya nchi ya Chile na manukato mengine (kwa kiasi fulani sawa na ile pilipili ya poda ya kusini magharibi mwa Marekani), ni "ingredient" muhimu inayotumika katika vyakula vingi. Pia muhimu ni niter kibbeh, siagi inayochanganishwa na tangawizi, vitunguu, na manukato kadhaa.
Vitoweo vyote vya wat huanzia vitunguu vyekundu vilivyokatwakatwa kwa kiasi kikubwa, ambavyo mpishi huvipika lakini visichemke au "sautees" katika sufuria. Mara tu vitunguu vinyookapo, mpishi huongeza niter kebbeh (au, kama ni vyakula vya vegan, huongeza mafuta ya mboga). Kufuatia hii, mpishi huongeza berbere kutengeneza keiy (Kiamhariki: ቀይ Key , Kitigrinya, Ge'ez: ቀይሕ ḳeyyi ḥ; "nyekundu")yenye manukato, wat au anaweza kuondoa berbere ili kuongeza ladha ya alicha wat au alecha wat (Kiamhariki: አሊጫ ālič̣ā). Katika tukio ambalo berbere hasa lina manukato, mpishi anaweza kuamua kuliongeza kabla ya kibbeh au mafuta ndiposa berbere liwezi kuiva kwa muda mrefu na kuwa na ladha. Mwishowe, mpishi huongeza nyama kama vile nyama ya ngombe(siga , Ge'ez: ሥጋ śigā ), kuku (Kiamhariki: ዶሮ dōrō , Kitigrinya: ደርሆ derhō ), samaki (Kiamhariki: asa ), mbuzi au kondoo (Kiamhariki: beg , Kitigrinya በግዕ beggi ʕ); kunde kama vile njegere (Kiamhariki: ክክ kik , Kitigrinya: ክኪ kikk ī) zilizopasuliwa au lentils (Kiamhariki: ምስር misi r, Kitigrinya: ብርስን birsin ); au mboga kama vile viazi es (dinich , Kiamhariki: ድንች dinič , Kitigrinya ድንሽ diniš ), karoti na chard (Kitigrinya: costa ).
Badala ya kuandaliwa kama kitoweo (stew), nyama au mboga zaweza kusautéed ili kutengeneza tibs (pia tebs , t'ibs , tibbs , nk Ge'ez ጥብስ ṭibs ). Tibs hupakuliwa kwa njia ya kawaida au njia maalumu, "tibs maalum" hupakuliwa juu ya chakula moto pamoja na mchanganyiko wa mboga (saladi). Katikati mwa karne ya 18 mgeni kutoka Ulaya aliyeitembelea Ethiopia, Remedius Prutky, alieleza tibs kama sehemu ya nyama iliyochomwa iliyopakuliwa "kuonyesha shukrani au kuonyesha heshima kwa mtu.
Chakula kingine cha Kiethiopia ni kitfo (mara nyingi huorodheshwa kama ketfo ), ambacho kina nyama mbichi (au nadra) ya ng’ombe iliyomarinateiwa katika mitmita (Ge'ez: ሚጥሚጣ mīṭmīṭā , poda ya pilipili iliyo na manukato nyingi) na niter kibbeh . Gored gored ni sawa na kitfo sana, lakini hutumia nyama uliokatwakatwa katika vipande vya boksi badala nyama uliosagwa.
Firfir au fitfit, (Ge'ez: ፍርፍር firfi r; ፍትፍት fitfit ) uliotengenezwa kutoka kwa vipande vya Injera pamoja na manukato, ni kiamsha kinywa cha kawaida. Kiamsha kingine maarufu ni dulet (Ge'ez: ዱለት dūlet ), mchanganiko wa manukato na "tripe"(laini ya nyama kutoka kwa ngombe,kondoo au mbuzi) , ini, nyama ya ng’ombe, na pilipili pamoja na Injera. Fatira inajumuisha pancake kubwa iliyokaagwa iliyotengenezwa kwa unga, mara nyingi huwa na safu ya yai, na huliwa kwa asali. Chechebsa (au kita firfir ) linafanana pankeki lililofunikwa na berbere na kibbeh , au manukato, na inaweza liwa kwa kijiko.
Tej ni mvinyo wa asali, sawa na Mead, ambayo mara nyingi huzolewa(serve) katika bars (hususan, katika tej bet ; Ge'ez ጠጅ ቤት ṭej bet , "nyumbani tej"). Katikal na araki ni mivinyo ambayo si ya bei ghali lakini zina nguvu.
Tella ni pombe aina ya bia ambayo hutengenezwa na huzolewa katika bars, ambazo pia huitwa "buna bets" (nyumba ya kahawa).
Kahawa (buna) ilianzia Ethiopia, na ni sehemu kuu ya vinywaji vya Ethiopia. Muhimu pia ni sherehe ambayo huandamana kuzolewa kwa kahawa, ambayo wakati mwingine huzolewa kutoka kwa jebena (ጀበና), mtungi wa udongo wa kahawa ambamo kahawa kuchemshwa. Katika nyumba nyingi eneo maalum la kahawa limezungukwa na nyasi, na lina samani maalum ya mtengenezaji kahawa. Sherehe iliyokamilika ina raundi tatu ya kahawa na ikiandamwa na uchomaji wa ubani.
Mesob (Ge'ez: መሶብ mesōb ) ni kifuniko cha meza ambacho chakula hupakuliwa. Mesob kwa kawaida huundwa kutoka kwa nyasi zilizokauka. Ina kifuniko ambayo huwekwa juu yake hadi muda wa kula unapowadia. Kabla chakula hakijakuwa tayari, beseni ya maji na sabuni ni huletwa nje kwa ajili ya kuosha mikono. Wakati chakula kimekuwa tayari, kifuniko huondolewa kutoka kwa mesob na chakula huwekwa katika mesob. Wakati mlo umeisha, beseni ya maji na sabuni huletwa ndiposa waliokula wapate nafasi ya kunawa mikono tena.
Chakula cha Gurage hutumia mmea wa uongo wa ndizi (enset , Ge'ez: እንሰት Inset ), aina ya ensete. Mmea huu husiagwa na kuwekwa kwa muda mrefu(ferment) ili kutengeneza chakula kinachofanana na mkate kinachoitwa qocho au kocho (Ge'ez: ቆጮ ḳōč̣ō ), ambacho huliwa pamoja na kitfo. Mzizi wa mmea huu unaweza kusiagwa kuwa poda na kuandaliwa kama kinywaji moto ambayo huitwa bulla (Ge'ez: ቡላ bula ), ambayo mara nyingi hupewa watu ambao wamechoka au wale ambao ni wagonjwa. Njia nyingine ya kuandaa Gurage ni kahawa yenye siagi (kebbeh ).
Mlo mkuu wa Gurage ambao ni maarufu sana ni kitfo. Gomen kitfo ni mlo mwingine ulioandaliwa katika tukio la Meskel, likizo maarufu linaloashiria ugunduzi wa Msalaba wa kweli. Sukuma wiki (ጎመን gomen ) huchemshwa, hukaushwa na kisha hukatwa vizuri na kupakuliwa pamoja na siagi, pilipili na manukato.
Gorsha ni tendo la urafiki. Kama ilivyosemwa hapo awali (juu), mtu hutumia mkono wake wa kulia kulirarua kipande cha Injera , kulibingirisha katika wat au kitfo , kisha kukiweka kipande hicho cha Injera kilichobingirishwa mdomoni. Katika mlo na marafiki, mtu anaweza kukirarua kipande cha Injera, kukibingirisha katika mchuzi, kisha kuweka kipande hicho cha Injera kinywani mwa rafikiye. Hii inaitwa gorsha , na ukubwa wa gorsha, huonyesha nguvu ya urafiki.
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.