ukarasa wa maana wa Wikimedia From Wikipedia, the free encyclopedia
Tiketi (pia: tikiti, kutoka Kiingereza "ticket") ni kipande cha karatasi au kadi inayoidhinisha mtu kuingia, kushiriki, kutumia au kusafiri. Tiketi huuzwa moja kwa moja au kidijitali siku ya matumizi au siku kadhaa kabla ya siku ya matumizi kufika.
Tiketi nyingine hushindaniwa au kutolewa bure kwa washiriki wakitimiza yanayohitajika au kama zawadi mtu anaponunua kitu au kulipa huduma fulani.
Kuna aina nyingi za tiketi, zikiwemo:
Bei za tiketi hutofautiana kulingana na tukio. Bei ya tiketi inaweza kuamuliwa kimataifa kama vile tiketi za ndege au kuamuliwa kitaifa na serikali ya kitaifa au mkoa kama vile tiketi za maonyesho ya kilimo, za kutembelea makavazi na mbuga za wanyama na sehemu nyinginezo zinazodhibitiwa na serikali. Bei ya tiketi zingine huamuliwa na mashirika husika au watu binafsi walio na wajibu wa kupanga tamasha zile. Bei ya tiketi hudhamiriwa na vitu mingi na hubadirishwa muda kwa muda.
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.