From Wikipedia, the free encyclopedia
Tausi (kwa Kilatini na Kiingereza Pavo) [1] ni jina la kundinyota dogo kwenye angakusi ya Dunia yetu lililopo kwenye ncha ya anga ya kusini.
Tausi lipo karibu na ncha ya anga ya kusini na jirani na makundinyota ya Darubini (en:Telescopium) upande wa kaskazini, Ndege wa Peponi (Apus) na Madhabahu (en:Ara) upande wa magharibi, Thumni (en:Octans) upande wa kusini na Mhindi (en:Indus) upande wa mashariki.
Tausi ni kati ya makundinyota yaliyobuniwa katika enzi ya kisasa. Kama nyota nyingi zinazoonekana kutoka nusutufe ya kusini pekee haikujulikana kwa Wagiriki wa Kale wala kwa Waarabu kwa hiyo wataalamu wa Ulaya hawakuwa na habari nazo. Kundinyota hili lilielezwa mara ya kwanza na mabaharia Waholanzi Pieter Dirkszoon Keyser na Frederick de Houtman katika safari yao ya kuelekea Indonesia ikaonyeshwa mara ya kwanza mwaka 1598 katika globu ya nyota ya Petrus Plancius na kupokelewa katika ramani za Johann Bayer.
Keyser alitumia jina la Kiholanzi "De Pauww" (Tausi) iliyotajwa baadaye kwa jina la Kilatini „Pavo“.
Leo Pavo - Tausi lipo pia kati ya makundinyota 88 yanayoorodheshwa na Umoja wa kimataifa wa astronomia [2] Kifupi chake rasmi kufuatana na Ukia ni 'Tau'.[3]
Nyota za Tausi ni chache na dhaifu; lakini kuna moja angavu inaitwa Peacock au a Alfa Pavonis yenye mwangaza unaoonekana wa mag 1.94 ikiwa na umbali wa miakanuru 179 kutoka Dunia[4].
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.