Kiharusi (kwa Kiingereza stroke) ni ugonjwa unaoleta hali ya mwili kupooza kutokana na matatizo kwenye mishipa ya damu inayolisha ubongo.

Ukweli wa haraka Stroke, Kundi Maalumu ...
Stroke
Mwainisho na taarifa za nje
Kundi MaalumuNeurology, neurosurgery Edit this on Wikidata
ICD-10I61.-I64.ner
ICD-9434.91
OMIM601367
DiseasesDB2247
MedlinePlus000726
eMedicineneuro/9 emerg/558 emerg/557 pmr/187
MeSHD020521
Funga

Katika tiba kiharusi ni upotevu wa uwezo wa ubongo unaoendelea haraka. Sababu yake ni tatizo katika mishipa inayopeleka damu kwenda ubongo.

Matatizo hayo ni ama kuzibwa ama kupasuka kwa mishipa ya damu. Seli za ubongo hufa haraka zisipopata oksijeni na lishe ya kawaida ambayo yote haya hufika kwa njia ya damu. Kiharusi ni hali ya dharura inayoweza kutibiwa kama tatizo linatambuliwa na kutibiwa haraka. Lisipotibiwa husababisha viwango mbalimbali vya kipooza mwilini.

Shinikizo la juu la damu, kisukari, chakula chenye mafuta mengi au kuvuta sigara huongeza hatari ya kupatwa na kiharusi.

Ufasiri na dalili

Kiharusi, ambacho pia hujulikana kama ajali ya ubongo na mishipa (CVA), chukizo la ubongo na mishipa chukizo (CVI), au shambulizi la ubongo, ni pale ambapo hali duni ya mtiririko wa damu kwenye ubongo husababisha kufa kwa kiini uhai.

Kuna aina mbili za kiharusi: cha iskemia kufuatia ukosefu wa mtiririko wa damu na cha kuvuja damu kufuatia kuvuja damu. Hali hizi husababisha kutofanya kazi vyema kwa sehemu ya ubongo.[1] Dalili zinaweza kujumuisha ukosefu wa uwezo wa kusogeza viungo au ukosefu wa hisia kwenye sehemu moja ya mwili, ugumu wa kufahamu au kuzungumza, hisia za kana kwamba dunia inazunguka au ukosefu wa uwezo wa kuona katika sehemu moja na kadhalika.[2][3] Kwa kawaida, lakini si kila mara, dalili hutokea haraka. Dalili zikidumu chini ya saa moja au mbili, hali hii hujulikana kama shambulizi la muda mfupi la iskemia (TIA).[3] Kiharusi cha kuvuja damu pia kinaweza kuhusishwa na hali kali ya maumivu ya kichwa.[3] Dalili za kiharusi zinaweza kuwa za kudumu.[1] Matatizo ya muda mrefu yanaweza kujumuisha niumonia au kupoteza uwezo wa kudhibiti kibofu.[3]

Visababishi, utambuzi na pathofisiolojia

Kipengele cha hatari kikuu cha kiharusi ni shinikizo la juu la damu.[4] Vipengele vingine vya hatari ni pamoja na kvuta tumbako, unene, wingi wa kolesteroli ya damu, kisukari, TIA ya awali, na mipigo ya moyo isiyo ya kawaida na kadhalika.[2][4] Kiharusi cha iskemia kwa kawaida husababishwa na kuzibwa kwa mshipa wa damu.[5] Kiharusi cha kuvuja damu husababishwa na kuvuja damu moja kwa moja kwenye ubongo au kwenye mwanya unaozunguka ubongo.[5][6] Damu inaweza kuvuja kufuatia kuvimba kwa msihipa ya ubongo.[5] Kwa kawaida utambuzi hufanywa kwa upigaji picha wa kimatibabu kama vile mchanganuo wa CT or mchanganuo wa MRI pamoja na uchunguzi wa kimwili. Vipimo vingine kama vile elektrokadiogramu (ECG) na vipimo vya damu hufanywa ili kubaini vipengele vya hatari na kuondoa visababishi tarajiwa. Viwango vya chini vya damu vinaweza kusababisha dalili sawa.[7]

Kinga na tiba

Kinga inajumuisha kupunguza vipengele vya hatari na pengine kutumia aspirin, dawa za kupunguza kolesteroli, upasuaji wa kufungua mishipa ya ubongo kwa wagonjwa walio na matatizo ya kupunguka kwa wembamba, na warfarin kwa watu walio na hali ya mipigo ya moyo isiyo ya kawaida.[2] Kwa kawaida kiharusi huhitaji matibabu ya dharura.[1] Kiharusi cha iskemia kikitambuliwa katika saa tatu hadi nne na nusu kinaweza kutibiwa kwa dawa inayooweza kuvunjavunja tone gumu la damu. Aspirin inapaswa kutumiwa. Baadhi ya matukio ya kiharusi cha kuvuja damu yanaweza kutibiwa kwa upasuaji. Matibabu ya kujaribu kurejesha utendakazi hujulikana kama urekebishaji wa kiharusi na kwa kawaida hufanywa katika kitengo cha kiharusi; hata hivyo, vitengo hivi ni vichache katika sehemu nyingi duniani.[2]

Uenezi

Mwaka 2010, takriban watu milioni 17 walipata kiharusi na watu milioni 33 walikuwa wamepata kiharusi awali na walikuwa wangali hai. Kati ya 1990 na 2010, idadi ya visa vya kiharusi vilivyotokea kila mwaka vilipungua kwa takriban 10% katika mataifa yaliyostawi na kuongezeka kwa 10% katika mataifa yanayostawi.[8] Mwaka wa 2013, kiharusi kilikuwa cha pili kikuu cha kifo baada ya ugonjwa wa ateri ya moyo, kikisababisha vifo milioni 6.4  (12% ya idadi jumla).[9] Takriban vifo milioni 3.3 vilisababishwa na kiharusi cha iskemia huku vifo milioni 3.2 vikisababishwa na kiharusi cha kuvuja damu.[9] Takriban nusu ya idadi ya watu walio na kiharusi huishi kwa muda wa chini ya nusu mwaka.[2] Kwa kijumla, thuluthi tatu ya visa vya kiharusi vilitokea kwa watu wa umri wa zaidi ya miaka 65.[8]

Viungo vya nje

  • Stroke
  • Canadian Stroke Network Archived 14 Aprili 2021 at the Wayback Machine.
  • Registry of the Canadian Stroke Network Archived 27 Mei 2006 at the Wayback Machine.
  • StrokEngine Archived 13 Februari 2006 at the Wayback Machine. (McGill University, Montreal, Quebec, Canada) Focuses on stroke rehabilitation and interventions
  • Cerebrovascular disease and risk of stroke Archived 17 Mei 2008 at the Wayback Machine.
  • "What Happens During a Stroke". NLM. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2007-12-14. Iliwekwa mnamo 2007-04-15. video
  • American Stroke Association Archived 21 Oktoba 2009 at the Wayback Machine.
  • National Stroke Association
  • Heart and Stroke Foundation of Canada
  • The Stroke Association UK
  • "Heart Attack, Stroke and Cardiac Arrest Warning Signs," from the American Heart Association
  • National Stroke Association of Malaysia

Marejeo

Wikiwand in your browser!

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.

Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.