From Wikipedia, the free encyclopedia
Feleji isiopatadoa (kwa Kiingereza: stainless steel) ni aloi ya feleji yenye kiwango cha chromi ambayo ni kinga dhidi ya kutu inayosaidia kutoshika kutu haraka.[1] [2]
Feleji isiopatadoa haithiriwi na madoa, kutu, asidi na ulikaji kirahisi kama chuma au feleji ya kawaida. [3]
Tabia hii inapatikana kama aloi ya feleji ina kiwango cha angalau asilimia 11 za kromi, pia kiwango cha kaboni katika masi yake isizidi % 1.2.
Ilhali feleji ya kawaida inatendana na maji na oksijeni kuunda kutu ambayo ni tabaka usoni isiyo imara inayoelekea kuachana na feleji na hivyo kuendelea kuipunguza, kromi inatendana na oksjeni kuunda tabaka jembamba sana ya oksidi ya chromi ambayo ni ngumu ilhali haiachani na feleji yenyewe. Hivyo inaunda tabaka imara inayozuia sehemu za feleji chini yake kuathiriwa.
Kuna aina tofautitofauti za feleji isiopatadoa; inawezekana kuunga madini mengine katika aloi; nyongeza za nikeli au molibdeni katika aloi zinaweza kuongeza uwezo wa kudumu katika mazingira penye asidi fulani au chumvi nyingi.
Namna ya kuongeza au kupunguza viungo katika aloi inabadilisha pia tabia nyingine kama uthabiti dhidi ya aina tofauti za shinikizo, ugumu, kiwango cha kuvunjika
Feleji isiopatadoa ilianza kutambuliwa katika karne ya 19 lakini wakati ule teknolojia haikupatikana bado kwa uzalishaji wake; tangu mwanzo wa karne ya 20 ilianza kutengenezwa katika viwanda.
Uzalishaji wake duniani kote kwenye mwaka 2018 ulikuwa tani milioni 50.7[4]
Feleji isiopatadoa ina faida nyingi hivyo matumizi yake yameenea sana.
Feleji hiyo haiwezi kutumiwa kwa shughuli zote kwa sababu inavunjika rahisi zaidi kuliko feleji ya kawaida pia haivumilii aina mbalimbali za shinikizo.
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.