Siku ya Bwana
From Wikipedia, the free encyclopedia
Siku ya Bwana (kwa Kigiriki, κυρακή ἡμέρα, "kyurakee eemera"; kwa Kilatini, Dominica dies) ni jina ambalo Wakristo wa lugha mbalimbali wanalitumia kutaja Jumapili.

Jina linapatikana katika kitabu cha mwisho cha Biblia ya Kikristo, Ufunuo (1:10).
Chanzo chake ni kwamba ndiyo siku ya juma ambayo wanasadiki Yesu alifufuka kutoka wafu. Hivyo ndiyo mwanzo wa uumbaji mpya wa vyote katika utukufu wake.
Kwa msingi huo, wengi wao wanaiheshimu kama siku muhimu zaidi kwa ibada zao, hasa kwa adhimisho la ukumbusho wake aliloliagiza akiwa katika karamu ya mwisho.
Ushuhuda wa kwanza wa desturi hiyo unapatikana katika Matendo ya Mitume (20:7).
Katika maandishi ya karne ya 2 BK, kwa mfano yale ya Yustino mfiadini, inaonekana desturi hiyo ilivyokuwa imeenea.
Marejeo
- From Sabbath to Lord's Day: A Biblical, Historical and Theological Investigation, D.A. Carson, editor (Grand Rapids, Mich.: Zondervan, 1982).
- The Study of Liturgy, Cheslyn Jones, Geoffrey Wainwright, Edward Yarnold, SJ, and Paul Bradshaw, editors (New York, N.Y.:Oxford University Press, 1992), pp. 456–458.
Viungo vya nje
- Dies Domini, Pope John Paul II, On Keeping the Lord's Day Holy Ilihifadhiwa 12 Mei 2019 kwenye Wayback Machine.
- Sabbath and Sunday in Early Christianity, Part 3: Irenaeus, and "the Lord's Day" Ilihifadhiwa 13 Mei 2013 kwenye Wayback Machine.
- Francis Turretin, On the Lord's Day Ilihifadhiwa 7 Mei 2006 kwenye Wayback Machine.
![]() |
Makala hii kuhusu dini ya Ukristo bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Siku ya Bwana kama historia yake, matokeo au athari zake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.