From Wikipedia, the free encyclopedia
Mchanga ni punje ndogo za mwamba uliosagika.
Kufuatana na mapatano ya kitaalamu mawe huitwa "mchanga" kama punje zake ziko kati ya milimita 0.063 hadi 2.
Punje hizo zinatokana na mmomonyoko wa mawe makubwa zaidi kama changarawe yaliyosukumwa na upepo au maji kwa mfano mtoni, baharini au kwenye mteremko wa mlima.
Jina mchanga halitaji mata yake lakini mara nyingi inamaanisha punje za silika (Si02) ambayo ni oksidi ya silikoni inayopatikana kwa wingi katika ganda la Dunia.
Mchanga hupatikana kwa wingi hasa kando ya bahari, jangwani au mtoni.
Mchanga ukichanganywa na saruji na maji huwa zege inayotumiwa kwa ujenzi.
Mchanga wa silika inaweza kuyeyushwa kuanzia jotoridi ya sentigredi 1713 na hivyo ni msingi wa kutengeneza kioo.
Makala hii kuhusu mambo ya sayansi bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mchanga kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.