From Wikipedia, the free encyclopedia
Rubidi (Kilat. rubidus: nyekundu) ni elementi na metali alikali yenye namba atomia 37 kwenye mfumo radidia na uzani atomia 85.4678. Alama yake ni Rb.
Rubidi (Rubidium) | |
---|---|
Rubidi ndani ya tubu katika angahewa ya arigoni | |
Jina la Elementi | Rubidi (Rubidium) |
Alama | Rb |
Namba atomia | 37 |
Mfululizo safu | Metali alikali |
Uzani atomia | 85.4678 |
Valensi | 2, 8, 18, 8, 1 |
Densiti | 1.532 |
Ugumu (Mohs) | {{{ugumu}}} |
Kiwango cha kuyeyuka | 312.46 K (39.31 °C) |
Kiwango cha kuchemka | 961 K (688 °C) |
Asilimia za ganda la dunia | 0.3 % |
Hali maada | mango |
Kali (potasiamu) ni metali laini sana inayochemka kwa sentigredi 39 tayari. Rangi yake ni nyeupe-fedha. Haipatikana kiasili kama metali tupu kwa sababu humenyuka haraka na kuoksidika hewani. Inamenyuka vikali sana na oksijeni na kuwaka peke yake ikiwekwa hewani tu.
Rubidi hutokea kwa umbo la isotopi mbili; 85Rb ni thabiti lakini 87Rb ni mnururifu na kugeuka kuwa 87Sr. Lakini nusumaisha yake ni miaka bilioni 48 hivyo unururifu ni mdogo.
Kutokana na uhaba wa metali kuina matumizi chache tu hasa katika utafiti wa kisayansi.
Makala hii kuhusu mambo ya kemia bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Rubidi kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.