From Wikipedia, the free encyclopedia
Ndoto ya Chumba Chekundu ni riwaya kutoka nchini China iliyotungwa katikati ya karne ya 18. Inahesabiwa kati ya riwaya 4 muhimu zaidi katika fasihi ya China. Mwandishi wake alikuwa Cao Xueqin (kwa Kichina: 曹雪芹).
,
Riwaya inasimulia habari za familia ya kikabaila ya Jia, mafanikio na hatimaye anguko lao.
Kenye kitovu cha masimulizi iko hadithi ya Jia Baoyu anayelelewa katika nyumba ya wazazi matajiri. Ana maisha mema bila mahangaiko kuhusu riziki zake; hahitaji kufanya kazi. Lakini haridhiki na maisha na hatimaye anaachana na dunia na kuwa mtawa.
Uhusiano wake na wanawake walio muhimu maishani mwake unasimuliwa kwa upana. Kutokana na nafasi kubwa ambayo wanawake wanapewa, riwaya hii imeitwa ya kifeministi.
Watendaji wengi wa riwaya wanaonyeshwa wakiwa vijana na hivyo kitabu hiki kilipendwa sana na vijana wa China kabla ya mapinduzi ya utamaduni.
Lugha ya Ndoto ya Chumba Chekundu ilikuwa lugha ya kawaida jinsi watu walivyosema kati yao, si lugha iliyotazamiwa kuwa sanifu wakati ule ambayo haikutumiwa katika majadiliano.
{{cite book}}
: Invalid |ref=harv
(help){{cite book}}
: Invalid |ref=harv
(help){{cite book}}
: Invalid |ref=harv
(help)Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.