From Wikipedia, the free encyclopedia
Katika hisabati, namba shufwa ni namba kamili inayogawanyika kwa 2 bila kuacha baki. Kama si vile, ni namba witiri.
Kwa hiyo jumla ya namba kamili hugawiwa katika makundi mawili yenye idadi sawa za namba. Kwa mfano kuanzia moja hadi kumi namba shufwa na witiri zinapokezana na zinaendelea mfululizo vile bila mwisho: 1, 2, 3, 4, 5, 6, 7, 8, 9, 10
Kwa mfano 6 ni shufwa kwa sababu hakuna baki tukiigawanya kwa 2: , bila baki.
Kinyume chake 3, 5, 7, 21 ni witiri kwa sababu zinaacha baki la 1 baada ya kuzigawanya kwa 2.
, inabaki 1
, inabaki 1
, inabaki 1
Mifano ya namba shufwa ni −4, 0, 8 na 1734. Mifano ya namba witiri ni −5, 3, 9 na 73.
Namba shufwa huwakilishwa na mlinganyo ufuatao:
ambapo s ni namba shufwa, na k ni namba kamili. Vilevile namba witiri huwakilishwa na mlinganyo:
ambapo w ni namba witiri. Hivi tunaweza kuchanganua kuhesabu kwa namba shufwa na namba witiri. Tokeo la kujumlisha au kutoa namba shufwa mbili, s1 na s2, ni:
2(k1±k2) ni shufwa, hivyo jumla ya namba shufwa mbili ni namba shufwa nyingine. Kujumlisha au kutoa namba shufwa na namba witiri ni kama hivi:
Jibu hili ni witiri. Kujumlisha au kutoa namba witiri mbili ni kama hivi:
Jibu hili ni shufwa. Mbinu huu unaweza kurudiwarudiwa kwa matendo mengine yote. Kwa ufupi:
Kwa ugawanyaji matokeo ni tofauti kwa sababu kugawanya namba kamili kwa namba kamili inaweza kuleta tokeo ambalo si namba kamili, kwa mfano , ambayo si namba kamili. Namba zisizo kamili si shufwa wala witiri.
Makala hii kuhusu mambo ya hisabati bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Namba shufwa na namba witiri kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.