Remove ads
From Wikipedia, the free encyclopedia
Mtaalamu wa anga ni mtaalamu wa masuala ya elimuanga (kwa Kiingereza: astronomy) au elimu ya anga-nje na violwa vya angani kama nyota, sayari, nyotamkia, na galaksi.
Kihistoria watu hao walitumia muda mwingi kuangalia nyota za anga kwa msaada wa vyombo kama darubini. Leo hii wataalamu wa anga hutumia hasa kompyuta na data kutokana na vipimo vya paoneaanga, vyombo vya anga-nje na darubini za angani.
Wataalamu wa anga wamesoma elimuanga ambayo ni tawi la pekee la sayansi, mara nyingi pamoja na kusoma matawi mengine ya sayansi kama fizikia, kemia, biolojia na kadhalika.
Wasichanganywe na majusi ambao husomea unajimu (kwa Kiingereza: astrology) na kutoa utabiri kuhusu maisha na tabia za watu kwa kuwa huo si tawi la sayansi yoyote, ingawa unadai kutegemea uchunguzi wa nyota n.k.
Makala hii kuhusu mambo ya fizikia bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mtaalamu wa anga kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.