From Wikipedia, the free encyclopedia
Nyanda za Juu za Mongolia ni sehemu za Nyanda za Juu za Asia ya Kati zinazoenea katika Mongolia na kaskazini mwa China kwa takriban kilomita za mraba 3,200,000. Inapakana na Milima ya Hinggan Kubwa upande wa mashariki, Milima ya Yin upande wa kusini, milima ya Altai upande wa magharibi, na milima ya Sayan na Khentii upande wa kaskazini. [1]
Ndani ya nyanda za juu liko Jangwa la Gobi na pia maeneo makubwa ya nyika kavu. Mwinuko uko takriban mita 1,000 hadi 1,500 juu ya u.b.
Kisiasa, eneo lote limegawanywa kati ya Mongolia, China na Urusi. Upande wa China, sehemu za Mongolia ya Kichina na mkoa wa Xinjiang ni sehemu ya nyanda za juu za Mongolia. Huko Urusi, ni sehemu za Buryatia na kusini mwa Irkutsk Oblast.
Nyanda za juu hizo zilikaliwa na kuvamiwa na vikundi mbalimbali katika mwendo wa historia, pamoja na Xiongnu, Xianbei, Waturuki wa Gök, nasaba ya Tang, nasaba ya Liao, Milki ya Wamongolia, na nasaba ya Qing.
Tabianchi inazidi kuwa yabisi. Maziwa mengi kwenye Nyanda za Juu za Mongolia kama vile Qagaan Nurr na Ziwa la XinKai, yamepungua kwa theluthi mbili za eneo lake la uso. Mengine yamekauka kabisa; Huangqihai na Naiman Xihu yamekauka kabisa kati ya miaka 1980 na 2010. Wakati maziwa machache kama vile Ziwa la Mashariki la Juyan na Had Paozi yamekoma, kwa wastani eneo lote la maziwa limepungua kwa 30%. [2] [3]
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.