From Wikipedia, the free encyclopedia
Mohenjo-Daro [1] ilikuwa mji mkubwa katika ustaarabu wa Indus uliostawi kwenye bonde la Mto Indus. Iko katika jimbo la Sindh, Pakistan ya leo.
Mji ulijengwa mnamo mwaka 2600 KK na kuwa kati ya miji ya kwanza duniani inayojulikana. Mohenjo-Daro ilistawi wakati mmoja na tamaduni za Misri ya Kale na Mesopotamia.
Mabaki ya mji yamepokewa katika orodha ya Urithi wa Dunia ya UNESCO.
Mohenjo-Daro ilijengwa mnamo karne ya 25 KK.[2] Ilikuwa kati ya miji mikubwa ya utamaduni wa Harappa ulioenea katika bonde la mto Indus. [3] Utamaduni huo ulianza mnamo mwaka 3000 KK na kuenea juu ya sehemu kubwa za Pakistan na Uhindi ya Kaskazini ya leo. Miji muhimu iliyotambuliwa na wanaakiolojia ilikuwa Harappa, Mohenjo-Daro, Lothal, Kalibangan, Dholavira na Rakhigarhi.
Mohenjo-Daro ilikuwa mji mkubwa wa Zama za Shaba yaani kipindi ambapo watu walikuwa wameshaanza kutumia metali badala ya zana za mawe tu lakini bado hawakutumia chuma.
Wataalamu wametambua kiwango cha juu wa kupangwa kwa mji huu. Wajenzi wake walitumia tayari matofali yaliyosanifishwa kwa kutumia vipimo vya sentimita 6 × 13 × 27.
Mji wote ulikuwa na mfumo wa visima vya maji zaidi ya 700 na pia mifereji kwa maji machafu. Watu wake walikuwa pia na mwandiko ambao haujatafsiriwa. [4]
Mnamo mwaka 1900 KK utamaduni wa Harappa uliporomoka kwa sababu ambazo hazikueleweka bado na wakazi waliondoka mjini.[2][5]
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.