From Wikipedia, the free encyclopedia
Milima kunjamano (kwa Kiingereza fold mountains) ni aina ya milima ambayo hutokea wakati mabamba ya gandunia yanagongana. Shinikizo linasababisha kukunjwa kwa ganda la dunia na hili linafanya sehemu ya uso wa ardhi kuinuliwa juu.
Tokeo lake ni safu ya milima au pia mfululizo wa masafu yaliyo sambamba.
Milima kunjamano ni umbo la kawaida kati ya milima mirefu duniani. Mifano ni milima ya Atlas katika Afrika ya Kaskazini, Alpi katika Ulaya na Himalaya katika Asia. Kilimanjaro ni mlima mrefu kwa upande wa Afrika lakini si mlima kunjamano kwa sababu ni volkeno ya pekee.
Makala hii kuhusu mambo ya sayansi bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Milima kunjamano kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.