Mwanzi (nyasi)

From Wikipedia, the free encyclopedia

Mwanzi (nyasi)

Mwanzi ni jina la spishi nyingi za nyasi ndefu zinazoweza kuonekana kama miti. Mianzi yote huwa na shina ya aina ya ubao.

Maelezo zaidi Uainishaji wa kisayansi, Ngazi za chini ...
Mwanzi
(Bambuseae)
Thumb
Msitu wa mianzi huko Japani
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Plantae (Mimea)
(bila tabaka): Angiospermae (Mimea inayotoa maua)
(bila tabaka): Monocots (Mimea ambayo mche wao una jani moja)
(bila tabaka): Commelinids (Mimea kama jaja)
Oda: Poales (Mimea kama manyasi)
Familia: Poaceae (Mimea iliyo mnasaba na manyasi)
Nusufamilia: Bambusoideae
Ngazi za chini

Makabila 3:

Funga

Mianzi hupatikana kiasili katika Afrika, Amerika na Asia lakini inastawi pia ikipandwa Ulaya.

Urefu wa spishi kubwa hufikia kina cha mita 40. Inaweza kukua zaidi ya mita 1 kila siku lakini kwa kawaida ni sentimita 3-5 kwa siku.

Shina la mianzi huwa na umbo la bomba na unene wake ni hadi sentimita 30. Shina hugawiwa na vifundo. Kila kifundo kina chipukizi na machipukizi yanaweza kuendelea kuota matawi.

Matumizi

Mianzi ina matumizi mengi kwa binadamu. Inafaa kwa ujenzi wa nyumba, madaraja au maboti. Mashina hutumika pia kwa mabomba ya maji katika nyumba na kilimo.

Wakati ni changa na laini yaani kabla ya kuwa ubao mwanzi unafaa kama chakula baada ya kupikwa. Mtovu unakusanywa pia kama kinywaji hasa ulanzi.

Katika utamaduni wa China ya Kale vipande vya mianzi vilitumiwa kama bao za kuandika matini.

Nyuzi zake hutumika pia kutengeneza magodoro.

Tanbihi

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.