From Wikipedia, the free encyclopedia
Mgongo kati wa bahari (kwa Kiingereza: Mid-oceanic ridge, kifupi: MOR) ni safu ya milima ya kivolkeno kwenye sakafu ya bahari, mita elfu kadhaa chini ya uso wake. Milima hii inapatikana kwenye mpaka wa mabamba mawili ya gandunia yanayoachana na hivyo kuacha ufa ambako magma moto kutoka chini inapanda juu.
Wakati wa kutoka na kuingia katika maji, magma iliyo katika hali ya kiowevu huganda na kujenga safu ndefu ya milima ya kivolkeno. Katikati, kwenye kilele cha safu, mara nyingi kuna ufa kama mfereji ambako magma inazidi kupanda juu inapoanza kuganda na kuwa mwamba thabiti pande zote mbili za mfereji.
Kwa hiyo kwenye mistari ya migongo kati ya bahari hutokea mfululizo ganda jipya la Dunia. Mchakato huo huitwa upanuzi wa sakafu ya bahari (ing. seafloor spreading).
Migongo ya bahari inapatikana katika kila bahari kubwa. Sehemu kubwa zaidi katika mfumo huo ni Mgongo kati wa Atlantiki ambako Bahari Atlantiki inapanuka sentimita mbili kila mwaka.
Katika sehemu kadhaa volkeno zinazoanza kwenye sakafu ya bahari zinazidi kukua hadi kupotoka kwenye uso wa maji na kuunda visiwa baharini. Mifano ni pamoja na visiwa vya Azori na kisiwa cha Ascension katika Atlantiki.
Mfano maalumu usio kawaida ni kisiwa cha Iceland kilichoanza hivihivi lakini ni kikubwa kulingana na visiwa vingine vya aina hii. Huko sehemu ya mgongo kati wa Atlantiki imeinuliwa juu pamoja na ufa ambako magma iliyotoka nje wakati ulikuwepo bado chini ya bahari. [1]
Pale ambapo ufa kati ya mabamba gandunia na hivyo mgongo wa bahari zinatokea, bahari huwa mara nyingi na kina cha mita 2,600 hivi [2]
Hali halisi safu hizi za kivolkeno mara nyingi hazipo katikati ya beseni la bahari, kwa mfano kwenye Pasifiki ziko upande, karibu na pwani ya Amerika. Lakini safu iliyotambuliwa mapema ilikuwa Mgongo kati wa Atlantiki iliyounda lugha ya "mid-ocean ridge" yaani mgongo kati wa bahari na jina hili linaendelea kutumiwa hata kama siku hizi zinaitwa pia "oceanic ridges" pekee.[3]
Tabia za migongo hiyo hutofautiana kulingana na kasi ya kupanuka.
Kasi ya kupanuka kwa mgongo imepimwa kati ya milimita 10 hadi 200.[4] Mgongo unaopanuka polepole kama ule wa Atlantiki huwa juu zaidi na kuonyesha mtelemko mkali kuliko mgongo unaopanuka haraka kama ule wa Pasifiki ya Mashariki wenye mitelemko midogo.
Mgongo unaopanuka polepole (chini ya mm 40 kwa mwaka) mara nyingi huwa na bonde la ufa kubwa katikati lililokadiriwa kuwa na upana hadi km 10 – 20 na vilele vikali. [5] [6]
Kinyume chake, mgongo unaopanuka haraka (zaidi ya mm 90/mwaka) kama ule kwenye Pasifiki Mashariki hukosa bonde la ufa.[7]
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.