From Wikipedia, the free encyclopedia
George Gordon Byron, 6th Baron Byron (22 Januari 1788 – 19 Aprili 1824) alikuwa mshairi na mwandishi mashuhuri nchini Uingereza. Mara nyingi anatajwa kwa cheo chake cha kikabaila kama Lord Byron.
Alikuwa mrithi wa mali kubwa hivyo aliweza kuendesha maisha kufuatana na mapenzi yake tu. Alikuwa maarufu kwa wapenzi wake wengi. Pamoja na kuandika alisafiri mahali pengi katika nchi za Bahari ya Mediteranea.
Tangu 1816 alihamia Italia alipojiingiza katika kundo la kisiasa lililolenga kuanzisha mapinduzi dhidi ya utawala wa Austria katika Italia ya Kaskazini. Aliamriwa kukaa katika mji wa Pisa bila kibali cha kutoka nje akatumia muda kwa mashairi.
1823 alipokea wito kutoka Ugiriki akawa kiongozi wa jeshi la Wagiriki waliopigania vita ya Uhuru dhidi ya Waturuki Waosmani. Hapa alikufa 1824 baada ya kungonjeka. Wagiriki wanamkumbuka hadi leo kama msaidizi wa uhuru wao.
Makala hii kuhusu mwandishi fulani wa Ulaya bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu George Byron kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.