From Wikipedia, the free encyclopedia
Lev Nikolayevich Tolstoy (kwa Kirusi Лев Николаевич Толстой; 9 Septemba 1828 - 20 Novemba 1910) alikuwa mwandishi kutoka nchi ya Urusi.
Huhesabiwa kati ya wanariwaya bora wa fasihi duniani. Kati ya masimulizi yake makuu kuna Vita na Amani pamoja na Anna Karenina.
Tolstoy alizaliwa katika familia ya makabaila kwenye kijiji cha Yasnaya Polyana karibu na mji wa Tula. Familia yake ilikuwa na undugu na makabaila wengi na Aleksander Pushkin alikuwa binamu yake.
Mapema Tolstoy alibaki yatima kutokana na kifo cha wazazi wake, akalelewa na dada yake mkubwa.
Alianza kusoma lugha za Kiasia halafu sheria, lakini alipofikia umri wa miaka 20 aliacha masomo akaenda kuishi kwenye mashamba ya familia yake. Hapo alijikuta kama bwana wa familia za wakulima maskini aliokuwa amewarithi kama sehemu ya mali yake, wakiwa kama nusu watumwa jinsi ilivyokuwa kawaida kwa wakulima wengi wa Urusi wa siku zile, kumbe akajitahidi kuboresha maisha yao.
Kama mwanajeshi alishiriki katika vita vya Urusi kwenye Kaukazi na vita vya Krimea.
Alirudi kwake kama adui wa vita akaendelea kulaumu vita na mabavu kati ya watu akijenga imani yake kwenye mfano wa Yesu Kristo.
Imani hiyo ilileta baadaye ugomvi na Kanisa rasmi la Urusi (Waorthodoksi) lililotumia imani ya Ukristo kwa kubariki jeshi la taifa, wakati Tolstoy alikataa kushiriki vita tena.
Aliendelea kukataa kila aina ya kuua, kwa hiyo alikataa kuchinja wanyama na kula nyama. Aliandika:
Mwaka 1862 alimwoa Sofia Andreevna Bers akazaa naye watoto 13.
Kutokana na vitabu vyake juu ya vita vya Krimea alikuwa maarufu nchini Urusi na riwaya kubwa zilizofuata zilijenga sifa zake za kimataifa.
Pamoja na riwaya aliandika pia juu ya dini. Kitabu "Ufalme wa Mungu umo ndani yenu" kiliathiri watu wengi, wakiwa pamoja na Mahatma Gandhi na Martin Luther King.
Mwaka 1910 alikufa kutokana na kifua kikuu akiwa na umri wa miaka 82.
Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Leo Tolstoy kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.