Remove ads

Lebanoni Ndogo (pia: Antilebanon) ni safu ya milima katika Lebanoni, Syria na Israel inayoelekea sambamba na milima ya Lebanoni yenyewe upande wa mashariki.

Thumb
Safu ya milima ya Lebanon

Kati ya safu hizo mbili liko bonde la Beka'a. Upande mwingine iko Dameski, mji mkuu wa Syria.

Safu ya Lebanoni ndogo ina urefu wa km 150. Milima mikubwa ni Hermoni (kwa Kiarabu: جبل الشيخ, jabal-ash-Shaikh) wenye kimo cha m 2,814 juu ya UB na Ta'a Musa (m 2,669).

Mpaka wa Syria na Lebanoni hufuata sehemu za juu za Lebanoni Ndogo.

Safu hiyo inazuia mawingu yanayobeba mvua kutoka Mediteranea kufika hadi eneo la Dameski.

Remove ads

Wikiwand in your browser!

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.

Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.

Remove ads