Mto wa Kongo (kati ya miaka 1971 na 1997 uliitwa zaidi "Zaire") ni mto mkubwa wa Afrika ya kati. Ni mto mrefu wa pili katika Afrika baada ya Nile. Pia ni mto wenye kina kirefu zaidi duniani. From Wikipedia, the free encyclopedia
Mto wa Kongo (kati ya miaka 1971 na 1997 uliitwa zaidi "Zaire") ni mto mkubwa wa Afrika ya kati. Ni mto mrefu wa pili katika Afrika baada ya Nile. Pia ni mto wenye kina kirefu zaidi duniani.
Chanzo | Katika milima ya Mitumba takr. 100 km magharibi ya Lumbumbashi (Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo) |
Mdomo | Atlantiki |
Nchi | Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Jamhuri ya Kongo |
Urefu | 4,700 km |
Kimo cha chanzo | 1,400 m |
Mkondo | 42,000 m³/s |
Eneo la beseni | 3,730,000 km² |
Idadi ya watu wanaokalia beseni | milioni 56 |
Miji mikubwa kando lake | Kisangani, Mbandaka, Kinshasa, Brazzaville, Matadi |
Beseni la Kongo pamoja na matawimto yake ni eneo kubwa la pili duniani la msitu wa mvua. Kwa kiasi cha mshuko wa maji mdomoni ni mto mkubwa wa pili duniani baada ya Amazonas (Amerika ya Kusini).[1]
Urefu wake ni kilomita 4,700 ukipimwa kuanzia chanzo cha tawimto la mbali zaidi ambalo ni mto Chambeshi wenye chanzo nchini Zambia. Mara nyingi urefu hutajwa kuanzia chanzo cha Lualaba halafu ni kilomita 4,374.
Jina la mto limetokana na Ufalme wa Kongo uliokuwa dola kubwa katika Angola ya Kaskazini na Kongo ya Magharibi wakati wa karne ya 14-17 BK. Jamhuri zote mbili za Kongo za leo zimepata majina yao kutoka mto huo.
Kuna taarifa ya mwaka 1535 kuhusu ufalme mdogo wa pili ulioitwa Kakongo kingdom. Ramani ya dunia iliyochorwa na Abraham Ortelius mnamo 1564 inaonyesha mji wa "Manicongo" kwenye mdomo wa mto kando ya bahari.
Jina la Bakongo kwa ajili ya jumla ya wasemaji wa lugha ya Kikongo ni jina la kisasa lililotumiwa tangu karne ya 20 tu.
Jina la pili linalotumiwa wakati mwingine ni "Zaire"; dikteta Mobutu Sese Seko alilifanya kuwa jina rasmi la mto pamoja na la taifa kati ya miaka 1971 - 1997. Jina hilo linatokana na neno la Kikongo "nzere" ("mto")[2].
Katika karne za 16 na 17 mto ulijulikana kwa majina yote mawili jinsi inavyoonekana katika maandishi ya siku zile, kwa mfano Mwingereza James Barbot aliandika mwaka 1746 juu ya safari kwenda mto "Kongo au Zaire" ("Voyage to Congo River, Or the Zair") [3]
Beseni la Kongo linalokusanya utiririshaji wa maji lina eneo la kilomita za mraba 4,014,500 [4]. Kongo inashusha (kutegemeana na majira na kiasi cha mvua) kila sekunde kati ya m³ 23,000 hadi 75,000 za maji kwenye Atlantiki (wastani umekadiria kuwa mita za ujazo 41,000 kwa sekunde)[5].
Kongo na matawimto yake inapita katika eneo kubwa la misitu ya mvua duniani (Amazonas pekee inapita katika msitu wa mvua mkubwa zaidi). Kwa kuwa ikipita pande zote mbili za ikweta, yaani kaskazini na kusini, sehemu fulani ya beseni lake huwa na majira ya mvua muda wowote.
Vyanzo vya Kongo viko katika nyanda za juu na kwenye milima inayopakana na Bonde la Ufa la Afrika ya Mashariki, pamoja na Ziwa Tanganyika na Ziwa Mweru ambayo yanamwaga maji kwenda mto Lualaba ulio tawimto kubwa zaidi la Kongo. Kwa kawaida chanzo cha mto Chambeshi huko Zambia, ambao unaishia katika Lualaba, huhesabiwa kama chanzo cha Kongo.
Lualaba inabadilisha jina lake mjini Kisangani ambako mto umepita maporomoko ya Bayoma na baada ya hapo huitwa Kongo. Mto unaelekea kaskazini, halafu mwendo wake unapinda kuelekea kusini magharibi, unapita mji wa Mbandaka unapopokea mto Ubangi halafu unaingia katika Bwawa la Malebo (kwa Kiingereza: Stanley Pool). Miji ya Kinshasa na Brazzaville inatazamana ikiwa pande mbili za bwawa hilo. Baada ya bwawa mto unakuwa mwembamba ukipita katika mabonde ya korongo kwenye idadi ya maporomoko inayojulikana kama maporomoko ya Livingstone Falls). Unapita miji ya Matadi na Boma (Kongo) na kuufikia baharini kwenye mji mdogo wa Muanda.
Matawimto yanaorodheshwa kuanzia mdomo kulekea chanzo. Kma namba zinatajwa zinaeleza urefu wa mwendo kwa kilomita (=km), eneo la beseni la tawimto kwa kilomita za mraba (=km²) na mshuko wa maji yaani kiasi cha maji kinachotoka mdomoni kwa mita za ujazo kwa sekunde (=m3/s)
Juu ya Miporomoko ya Boyoma karibu na Kisangani mto kongo hujulikana kwa jina la mto Lualaba.
Mto Kongo ni njia muhimu ya mawasiliano na biashara kwa meli zinazoweza kusafiri mle kwa kushirikiana na njia za reli penye maporomoko mahali patatu.
Maporomoko ya Livingstone yanazuia meli kupita kutoka baharini. Kuanzia Kisangani hadi Kinshasa mto ni njia ya maji inayopitiwa na meli za mtoni. Upande wa Lualaba kuna sehemu kadhaa zinazofaa kwa meli lakini njia ya maji inakatwa mara kadhaa na maporomoko.
Sehemu kubwa ya bidhaa kwenda Afrika ya kati zinasafirishwa mtoni.
Mto Kongo ni mto wenye maji mengi katika Afrika yote. Hivyo kuna nafasi kubwa ya kuzalisha umememaji. Kama nafasi zote zingetumika ingewezekana kutosheleza mahitaji yote ya umeme kwa Afrika kusini kwa Sahara. [6]
Hadi sasa kuna takriban vituo 49 vinavyozalisha umememaji katika beseni la Kongo. Kituo kikubwa kiko kwenye Lambo la Inga takriban kilomita 200 upande wa kusini magharibi wa Kinshasa. Mradi ulianzishwa katika miaka ya 1970. Wakati ule mfululizo wa malambo 5 ulipangwa. Hadi sasa 2 yamejengwa, lambo la kwanza (Inga I) lilikuwa tayari mwaka 1972, Inga II ikafuata mwaka 1982 na yote miwili ina rafadha 14[6] zinazoweza kuzalisha megawati 1,775 kwa jumla, lakini kutokana na uhaba wa matengenezo na usimamzi yanafikia si zaidi ya nusu yake. [7]
Shirika la Eskom kutoka Afrika Kusini imependekeza kuongeza lambo la tatu na - pamoja na matengenezo kwenye malambo mengine - kuongeza uwezo wa majiumeme hadi kiwango cha gigawati 40. [8]
Lakini kuna wataalamu walioonyesha mashaka kuwa malambo mapya yatakuwa hatari kwa ekolojia ya mto na hasa maisha ya spishi nyingi za mtoni.[9]
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.