Kisiwa cha Kome

From Wikipedia, the free encyclopedia

Kisiwa cha Kome ni kati ya visiwa vya mkoa wa Mwanza, kaskazini mwa Tanzania.

Kinapatikana katika ziwa Nyanza, la pili duniani kwa ukubwa, maarufu zaidi kama Ziwa Viktoria.

Kisiwa kinakaliwa na watu toka makabila mbalimbali ya Tanzania; muingiliano huo unatokana na shughuli za uvuvi, hivyo maeneo kama Ntama, ambacho ndicho kitovu cha kisiwa, Mchangani, Nyalusenyi na Kabaganga yanaongoza kuwa na muingiliano mkubwa wa watu.

Wenyeji ni Wazinza. Japo Wasukuma na makabila mengine yapo kwa wingi pia.

Upatikanaji wa chakula ni wa kuridhisha haswa kwa kuwa wakazi ni wakulima na ardhi ni nzuri yenye rutuba na upande wa kitoweo wakazi ni wafugaji wadogowadogo na wavuvi, hivyo vitoweo ni vya kutosha.

Tazama pia

Tanbihi

Viungo vya nje

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.