Kiajemi (au Kifarsi, فارسی; au Kiparsi, (پارس) ni lugha ya taifa ya Uajemi. Ni kati ya lugha za Kihindi-Kiajemi, ambazo tena ni kati ya lugha za Kihindi-Kiulaya.
Inaandikwa kwa herufi za Kiarabu ambamo herufi nne za ziada zimeongezwa kwa kutaja sauti zisizoweza kuonyeshwa kwa Kiarabu asilia. Hizo herufi za ziada ni پ p, چ ch, ژ zh na گ g.
Kiajemi kilikuwa na athira kubwa juu ya lugha mbalimbali hasa Kiarabu na Kituruki, lakini pia Kiswahili.
Kuna wasemaji wa lugha ya kwanza milioni 70, na takriban wasemaji wengine milioni 60 kama lugha ya pili. Inatumiwa hasa katika nchi zifuatazo:
- Uajemi (Iran)
- Tajikistan
- Afghanistan
- Katika Afghanistan, yenye wasemaji takriban milioni 15, lugha inaitwa "Kidari" (درى).
- Katika Tajikistani, yenye wasemaji milioni 15 pia, lugha inaitwa "Kitajiki".
Kutokana na uhamiaji wa karne ya 20 lugha inapatikana katika nchi nyingi za dunia.
Viungo vya nje
Wikiwand in your browser!
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.