From Wikipedia, the free encyclopedia
Kelvini ni Kizio cha SI kwa halijoto. Alama yake ni K.
Kiwango chake kinaanza kwenye sifuri halisi (= -273.15 °C) pasipo mwendo wowote wa molekuli. Kizio kimoja cha Kelvini ni sehemu ya 1/273.16 ya tofauti kati ya sifuri halisi (=0 K) na kiwango utatu cha maji (+0.01 °C).
Skeli ya Kelvini ililinganishwa na skeli ya selsiasi yaani kizio kimoja cha Kelvini ni sawa na kizio kimoja cha Selsiasi.
Skeli ya Kelvini haina namba hasi (-) kwa sababu hakuna hali chini ya 0 K.
Jina limetokana na mwanafizikia Mwingereza William Thomson aliyekuwa na cheo cha Lord Kelvin (1824–1907).
Makala hii kuhusu mambo ya sayansi bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Kelvini kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.