From Wikipedia, the free encyclopedia
Karakoram (pia Karakorum) ni eneo la milima mirefu inayopakana na Himalaya upande wa mashariki na Hindu Kush upande wa kusini; eneo hili lipo mpakani mwa Pakistan, Uhindi na China likienea hadi Afghanistan na Tajikistan.
Safu za Karakoram zinaenea kwa kilomita 482. Kuna milima mirefu minne yenye kimo juu ya mita 8,000 ambayo ni K2 (m 8.611), Gasherbrum I (m 8.080), Broad Peak (m 8.051) na Gasherbrum II (m 8.035).
Pia kuna barafuto mashuhuri kama vile Siachen na Biafo zinazoenea kwa kilomita 76 na 63.
Sehemu kubwa ya maji kutoka Karakoram huishia katika beseni la mto Indus na kuelekea nao kwenye Bahari Hindi.
(kimo kwa mita juu ya usawa wa bahari)
Makala hii kuhusu maeneo ya Asia bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Karakoram kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.